Windows

Simba vs Sevilla, mchezo wa kihistoria



Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo watashuka uwanja wa Taifa kumenyana na Sevilla katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa moja jioni na utarushwa mbashara na vituo vya televisheni zaidi ya 56 ambapo kwa upande wa Afrika, SuperSport itarusha mchezo huo mbashara

Licha ya kuwa mchezo wa kirafiki, lakini mchezo huo umevuta hisia za mashabiki wa soka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kutokana na ukubwa wa timu ya Sevilla

Hii ni mara ya kwanza kwa timu inayoshiriki ligi kuu ya Hispania, La Liga kufika Tanzania na hata Afrika Mashariki pia

Aidha rekodi ya Sevilla kwenye soka la Ulaya, itafanya mchezo huo kufuatiliwa na watu wengi

Mabingwa wa nchi, Simba waliwasili jana mchana kutoka Dodoma siku moja baada ya kutetea ubingwa waliotwaa msimu uliopita

Uongozi wa Simba umewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kupata burudani

Licha ya kufahamu ubora wa Sevilla, Simba imepania kuchuana na wababe hao wa soka la Ulaya na kupata ushindi ili kulitangaza jina la timu hiyo na Tanzania kwa ujumla

Kiingilio cha chini cha mchezo huo Mzunguuko ni Tsh 5,000/-wakati majukwaa ya VIP B nia Tsh 15,000/-

Pia kuna tiketi za Platinum ambazo zitapatikana kwa Tsh 100,000/-

Post a Comment

0 Comments