Kikosi cha Azam FC kimeanza rasmi mazoezi kwaajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi, Simba SC.
Mchezo huo muhimu kwa timu zote hasa Simba ambayo iko kwenye mbio za kutetea ubingwa wake, utapigwa Jumatatu Mei 13, 2019 kwenye Dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Ni mchezo wa kisasi kwa timu hizi kwani katika mchezo wa kwanza, Simba walipata ushindi wa mabao 3-1, hivyo Azam wanasaka heshima ya kulipa kipigo hicho.
Timu zote mbili hazikupata matokeo mazuri kwenye mechi zao zilizopita, Simba ikiwa imetoka kujeruhiwa kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar na Azam ikitoka kupata sare ya bila kufungana dhidi ya KMC kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi Complex.
Wakati Simba ikihitaji pointi tisa pekee katika mechi sita ilizobakiza kutetea ubingwa wake, Azam inahitaji ushindi ili kujiongezea pointi katika nafasi yake ya tatu ikiwa imesalia na mechi tatu pekee.

0 Comments