

KESHO kikosi cha Simba kitamenyana na Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine ikiwa ni mchezo wao wa 30 kwenye ligi.
Mpaka sasa Simba ambao ni mabingwa watetezi wamejikusanyia jumla ya pointi 75 wakiwa nafasi ya pili huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 80 akiwa amecheza michezo 34.
Wachezaji wawili ambao walikuwa majeruhi, nahodha, John Bocco na beki Pascal Wawa wanatarajiwa kuanza mazoezi na timu kesho huku Paul Bukaba akiwa nje ya mchezo kutokana na majeraha ya mguu aliyoyapata jana wakati wanamenyana na Mbeya City.



0 Comments