Sevilla inayodhaminiwa na Sportpesa mbali ya kucheza mechi hiyo dhidi ya Simba pia watafanya shughuli za kijamii pamoja na kliniki na mafunzo mbalimbali.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa ya La Liga, Oscar Mayo alisema katika ushindani wa kimataifa unakutana na dhamira ya LaLiga kuwa karibu na mashabiki wake.
“Mashabiki wetu wa Tanzania watapata furasa ya kuangalia karibu Sevilla FC inamaanisha kuwa ni fursa kubwa kwa kila mtu," alisema Mayo.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kampuni yao imeshirikiana na baadhi ya taasisi za soka za kubwa ulimwenguni baada ya kuna kuna haja ya kuleta uzoefu huu mkubwa kwa Tanzania.
"Ili kufurahia kuona moja ya klabu kubwa Ulaya, Sevilla FC. Kwa makubaliano yetu na LaLiga ambayo ni ligi bora duniani, tutaweza kuonyesha vipaji vyetu na kuboresha kiwango cha soka nchini," alisema Talimba.
Alisema mechi hiyo ni sehemu ya mradi wa 'LaLiga duniani ambao unalenga kueneza soka la Hispania kimataifa na kueneza pia sera ya 'Marca España', kuleta karibu mashabiki wa LaLiga na kukuza klabu nje ya nchi yetu.
Hii itakuwa ni klabu ya pili Ulaya kufanya ziara Afrika Mashariki, baada ya mwaka 2017, Everton FC kucheza na Gor Mahia nchini Kenya, ingawa sio mara ya kwanza kwa Sevilla kutua katika bara hili kwani mwaka 2015 ilikuwa nchini Morocco ambao ilicheza mechi ya kuajindaa na LaLiga dhidi ya Hassania Union Sport d'Agadir.
0 Comments