


MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohamed Salah, ametamba kuzitikisa nyavu za Tottenham katika mtanange wa fainali ya Ligi ya Mabingwa utakaochezwa keshokutwa.
Liver itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza fainali iliyopita dhidi ya Real Madrid, ambayo walichapwa mabao 3-1.
Akizungumza na kituo cha runinga cha beIN Sports, nyota huyo alisema anajivunia kupata nafasi nyingine ya kuingia hatua hiyo ya fainali.
“Naamini nitacheza mechi yote na kufunga bao muhimu la ushindi. Tutasahihisha makosa yaliyofanyika katika fainali iliyopita dhidi ya Madrid,” alisema Salah.
Itakumbukwa kuwa Salah alishindwa kumaliza dakika 90 za mechi hiyo dhidi ya Madrid baada ya kuumizwa bega na Sergio Ramos.



0 Comments