Windows

Robert Marawa, mtangazaji maarufu SuperSport afutwa kazi


Kwa wanaofuatilia michuano mbalimbali ya soka ndani na nje ya Afrika kupitia kituo cha televisheni cha Supersport watamfahamu mtangazaji mahiri Robert Marawa ambaye ametimuliwa kazi katika kituo hicho
Inaelezwa chanzo cha kutimuliwa kwake kinatokana na ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akiituhumu Supersport kuajiri baadhi ya wafanyakazi wake ambao wanatuhuma za unyanyasaji wa kijinsia
Hata hivyo Supersport katika ukurasa wao wa mtandao wa Facebook pia waliandika kuwa wanatarajia kufanya mabadiliko ya watangazaji hasa watangazaji wa ndani na pia wataangalia marekebisho ya mkataba wa Marawa
Marawa anadai kupokea ujumbe kwa njia ya simu kutoka kwa Bosi wa Supersport ambao ulimueleza kuwa amefutwa kazi
Mwananchi wengi nchini Afrika Kusini wamepinga utaratibu uliotumika kumfukuza mtangazaji huyo mkongwe aliyejiung na kituo hicho mwaka 2006

Post a Comment

0 Comments