

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho amesema matatizo ya timu hiyo hayatokani na wachezaji, bali ni mfumo mzima wa uendeshaji wa timu
Mourinho alitimuliwa kazi mwezi Disemba 2018 nz nafasi yake kuchukuliwa na Ole Gunnar Solskjaer akiwa kocha wa muda
Hata hivyo kocha huyo hakufanya maajabu yoyote licha ya kuanza vizuri wakati akikaimu nafasi hiyo kwa kushinda michezo 10 kati ya 11
Tangu ateuliwe rasmi kuwa Meneja mwezi Machi, Sokljaer amesuasua Manchester United ikishinda mechi mbili tu kati ya tisa za mwisho na kujikuta ikimaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi
cut
"Sitaki kuonekana kuwa mtu mzuri "Mourinho ameliambia gazeti la Ufaransa L'Equipe.
"Kwa sababu mtu 'huyo mzuri' baada ya miezi mitatu amekuwa kibaraka ambapo mwisho wake hauwezi kuwa mzuri".
"Kuna wakati mwingine ni kama uko peke yako na hakuna ambaye anakuunga mkono katika klabu, wakati mwingine wachezaji wanatofautiana na kocha , je nani ni mtu mzuri?"
Katika mahojiano na gazeti hilo, amesema "msimu wangu wapili ulikuwa ulikuwa mzuri, ninasema hivyo kwa sababu tulitimiza malengo tuliojiwekea."
"Niliwakamua wachezaji kama machungwa ili tupate matokeo."
Kocha huyo amesema matatizo ya Manchester United ni ya kimfumo na hayaishii tu kwa wachezaji watukutu kama Paul Pogba.
Aidha Mourinho amesema hakuwahi kuwa na matatizo na kiungo Paulo Pogba



0 Comments