Windows

Ajib apewa nafasi ya kuamua hatma yake Yanga


Uongozi wa Yanga umewahakikishia wachezaji wake kuwa unatambua mchango wao kwa klabu hiyo msimu huu na kuwahakikishia changamoto zilizojitokeza hazitakuwepo msimu ujao
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema timu hiyo imekusudia kuwabakisha wachezaji wote waliopendekezwa na kocha Mwinyi Zahera kwa ajili ya kukipiga kunako klabu hiyo msimu ujao
Hata hivyo amesema kwa wale ambao mikataba yao inamalizika, uamuzi wa mwisho unabaki kwao
Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo kuungana na waajiri wake wa zamani Simba
Hata hivyo Dk Msolla amesema Ajib yuko kwenye mipango ya kocha Zahera kwa ajili ya msimu ujao
"Ajibu ni mchezaji wetu na malengo ni kuendelea kubaki hapa Yanga ndiyo maana tunatafuta fedha kwa bidii kuona wachezaji wetu wanakuwa imara msimu ujao ingawa ni uamuzi wake kuondoka na lazima ajipime na kujitafakari mwenyewe," amesema Dk Msolla
"Tunapambana kuona msimu ujao tunakuwa na wachezaji ambao watakuwa imara na kutengeneza timu yenye ushindani kwenye ligi"
Juzi uongozi mpya wa Yanga ulikutana na wachezaji wote katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya klabu hiyo, mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam
Ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa kujadili maslahi ya wachezaji hasa ikizingatiwa msimu wa unaelekea kumalizika katika kipindi cha wiki mbili zinazokuja



Post a Comment

0 Comments