KIPIGO cha 8-1 walichokipokea Coastal Union dhidi ya Simba kimewashtua wapenzi wa mpira nchini na kuanza kuhoji chinichini namna ambavyo wamekubali kipigo hicho.
Hata hivyo Mwanaspoti liliweza kuzinyaka za chini chini kwamba kikosi hiko kiliingia saa tatu asubuhi leo na saa kumi walishuka uwanjani kucheza na Simba.
Sababu kubwa inatajwa ni kutokana na timu yao ya Vijana kutumia gari ambalo linatumiwa na timu ya wakubwa. Kikosi cha vijana kinashiriki mashindano maalum ya TFF chini ya miaka 20 yanayoendelea nchini.
Mwanaspoti lilizungumza na kocha mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda na kukiri wamevuna walichokipanda.
"Kweli tumefika alfajiri sitaki kuwa mnafki na minazungumza ukweli katika hilo kabisa, wachezaji wangu walichoka," alisema. Aliongeza kwamba uchovu huo ulijionyesha zaidi katika kipindi cha pili ndipo wapinzani wao walitumia nafasi hiyo kupata magoli zaidi.
0 Comments