Washambuliaji Emmanuel Okwi na Medie Kagere wamepiga hat trick kila mmoja na kuizawadia Simba jumla ya mabao sita kutoka kwenye miguu yao na kuifanya timu hiyo kupanda kileleni kwa kufikisha alama 81.
Ushindi huo ni kama zawadi kwa kigogo wa timu hiyo, Mohamed Dewji ambaye siku ya leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mo aliandika ujumbe kuipongeza timu hiyo kwa ushindi iliupata ambapo alisema umempa furaha kwenye siku yake ya kuzaliwa.
Katika mchezo huo spidi aliyokuwa anaionyesha Okwi ilionekana kuwa mwiba kwa mabeki wa Coastal, Bakari Mwamyeto na Ibrahim Ame.
Katika kipindi cha kwanza Simba walianza kwa kushambulia na kuhitaji goli la mapema zaidi.
Ndani ya dakika 4 Simba walikosa nafasi zaidi tatu za wazi ambazo wangeweza kupata magoli.
Coastal Union walionekana kuelemewa na presha ya washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi ambao walionyesha kuwa na maelewano mazuri.
Dakika 10 Simba walipata goli baada ya Rashid Juma piga shuti na kipa wa Coastal, Soud Abdallah alitema na kukutana na Okwi aliyeweka mpira wavuni moja kwa moja.
Baada ya goli hilo liliwaamsha Coastal Union na kuanza kufunguka wakisogea kwa Simba kwa mashambulizi ya kushtukiza.
Dakika 14 mshambuliaji wa Coastal, Andrew Simchimba alipiga shuti na kugonga mwamba mabeki wa Simba waliokoa haraka.
Baada ya shambulizi hilo Simba nao walizidisha mbinu za kusogea kwa Coastal Union, ambapo walikuwa wakitumia upande wa Rashid Juma aliyekuwa anaonekana ana spidi.
Dakika 19 okwi alipigiana pasi za haraka haraka na kagere ambaye alimpenyeza Okwi na kuingia nao ndani ya 18 na kumpiga chenga kipa na kuweka mpira wavuni likiwa goli la pili.
Dakika 24 Raizin Hafidh alitaka kuifungia Coastal baada ya kupiga shuti lakini Manula alipangua na kuwa kkna isiyokuwa na faida.
Dakika 28 Coastal walifanya mabadiliko kwa kumtoa Said Jeilani na kuingia Prosper Mushi ili kwenda kuongeza nguvu katika eneo la kiungo.
Dakika 34 Raizin Khafidh aliifungia Coastal akiwa nje ya 18 baada ya kupiga shuti lililoenda moja kwa moja wavuni.
Raizin alionekana kuwa na umiliki mzuri wa mpira hali iliyowasumbua mabeki wa Simba katika kumkaba.
Dakika 46 Okwi alifunga goli la tatu baada ya Clatous Chama kupiga krosi na mabeki wa Coastal kushindwa kuelewana, Okwi aliweka mpira moja kwa moja wavuni akiwa ndani 18.
Coastal walifanya mabadiliko dakika 53 kwa kutoka Hija Ugando na kuingia Hamis Kanduru.
TAKWIMU:
Hii ni hat trick ya pili msimu huu kwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi. Hat trick yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Oktoba 28 mwaka jana ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-0. Pia ni hat trick ya tano msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hat trick nyingine msimu huu zimefungwa na Meddie Kagere, Fully Zullu Maganga wa Ruvu Shooting, Alex Kitenge aliyekuwa Stand United na Salim Aiyee wa Mwadui.
0 Comments