Windows

Okwi ataamua hatma yake mwenyewe - Rweyemamu



Meneja wa klabu ya Simba Patrick Rweyemamu amesema mshambuliaji wa timu hiyo Emmanuel Okwi ni miongoni mwa wachezaji 13 ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu hivyo ataamua hatma yake mwenyewe

Jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Okwi aliweka ujumbe ulioibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa Simba wengi wakijiuliza kama alikuwa akiondoka klabuni hapo

Rweyemamu amesema baada ya mchezo wa mwisho wa kumaliza msimu dhidi ya Mtibwa Sugar kesho, hatma za wachezaji ambao mikataba yao inamalizika, itafahamika

"Mwenye kauli ya mwisho na iliyokamika ni yeye mwenyewe Emmanuel Okwi, mimi siwezi kumzungumzia kwa sababu bado tuna mechi Jumanne na kesho (leo) kikosi kamili kinaelekea mjini Morogoro," amesema Rweyemamu

"Sio Okwi pekee, kuna wachezaji wengi takribani 12 au 13 wanamaliza mikataba yao na tutaangalia uhitaji wa benchi la ufundi wao ndio watatoa mapendekezo ya wachezaji wanaoondoka na wanaobaki"cut

Okwi amekuwa akihusishwa na timu kadhaa kutoka Afrika Kusini

Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Uganda ni kawaida yake 'kuwa mtata' anapodai mkataba mpya wadadisi wa mambo wakiamini anafanya hivyo ili kuongeza dau lake la usajili

Uongozi wa Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo' amesema wachezaji wote waliopendekezwa na kocha Patrick Aussems kubaki Simba, wataongezewa mikataba

Nyota wa Simba ambao mikataba yao imemalizika ni pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Nicholas Gyan, Erasto Nyoni, James Kotei, Jonas Mkude, Haruna Niyonzima, John Bocco na Emmanuel Okwi

Inaelezwa Bocco tayari ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kubaki Msimbazi, juzi Mo pia alimalizana na kiungo Jonas Mkude

Post a Comment

0 Comments