Windows

Ajib anarudi nyumbani 'kumenoga'



Jana klabu ya TP Mazembe ilitangaza kuachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Yanga Ibrahim Ajib baada ya kushindwa kufikia makubaliano katika maslahi binafsi

Taarifa iliyotolewa na timu hiyo kwenda klabu ya Yanga imethibitisha kukwama kwa 'dili' hilo

Hata hivyo imeelezwa kuwa Ajib asingeweza kujiunga na Mazembe kwa kuwa tayari alishasaini mkataba wa awali kuitumikia Simba mwezi ujao

"Ajib alisaini Simba tangu mwezi uliopita na sehemu ya fedha za usajili wake tayari alishachukua. Mazembe wasingeweza kumsajili kabla ya kurudisha fedha za Simba" kilieleza chanzo cha habari kutoka ndani ya klabu ya Simba

Wiki iliyopita Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' alisema timu hiyo iko tayari kushindana na timu vigogo wa soka barani Afrika kusajili wachezaji wazuri

Mo amedhihirisha kauli yake kwa kuizuia Mazembe kumsajili Ajib

Post a Comment

0 Comments