

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema timu hiyo inafahamu kiungo wa Gor Mahia Francis Kahata mkataba wake unamalizika mwezi wa saba na ameshawaambia viongozi wa timu yake kuwa ataondoka
Hata hivyo Magori hajaweka wazi kama kiungo huyo fundi anayehusishwa kutua Msimbazi kama atasajiliwa
"Kahata amemaliza mkataba wake nafikiria amewaambia hawezi kuendelea kuchezea Gor Mahia, kama anakuja Simba mimi sifahamu. Hizo zote ni tetesi tu za usajili na zipo nyingi, tulieni tu usajili utawekwa hewani," amesema
Aidha Magori amefafanua kuwa usajili wa Simba utafanywa kulingana na mapendekezo ya benchi la Ufundi ambapo tayari wameshapokea ripoti ya kocha Patrick Aussems kuhusu maboresho ya kikosi chao
"Ripoti ya mwalimu tayari imeshafika na itawekwa wazi, Jumanne tuna mchezo wa mwisho wa ligi baada ya hapo kila mchezaji atajua hatma yake"
"Kuna ambao bado wanamikataba na wengine inaisha, wapo watakaoendelea na wengine hawataendelea na wengine bado mazungumzo yanaendelea baada ya Jumanne kila kitu kitakuwa wazi"
"Usajili unamambo mengi sana, si kila mchezaji ambaye mkataba unaisha anaachwa unaweza kuwa na mkataba na ukaachwa lakini huwezi kumwacha mchezaji wakati bado hujui anaekuja ni nani"
"Wakati mwingine kocha anasema hawa bado vijana watolewe kwa mkopo wakajifunze lakini hawa kama tutapata wachezaji bora zaidi yao basi waachwe waje wengine"cut
Kama Simba itamsajili kiungo huyo fundi, ataungana na viungo wengine mahiri katika kikosi cha Simba Clatous Chama, Haruna Niyonzima na Hassani Dilunga
Aidha Simba pia iko mbioni kumrejesha kiungo Ibrahim Ajib aliyemaliza mkataba klabu ya Yanga



0 Comments