Windows

Nahodha Sevilla aitabiria Simba makubwa Caf

NAHODHA na beki wa kulia wa Sevilla FC inayoshiriki La Liga ya Hispania, Jesus Navas amewatabiria makubwa Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mwaka huu.

 

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Simba uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Sevilla ya Hispania iliifunga Simba mabao 5-4.

Simba inatarajiwa kuiwakilisha nchi kwa mara ya pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuutetea ubingwa wao wa ligi kwa mara ya pili mfululizo. Akizungumza na Championi Jumamosi, Navas alisema siyo kitu kidogo kwa Simba kupata matokeo ya kufungwa mabao 5-4 na timu kubwa kama Sevilla inayoshiriki La Liga.

 

Navas ameipongeza Simba kwa matokeo hayo huku akiwatabiria kufanya vema kwenye michuano hiyo mikubwa watakayoshiriki Afrika.

 

“Hatukutarajia kukutana na ushindani huu tuliokuta kutoka kwa Simba, kiukweli wamecheza vizuri na kutupa changamoto nzuri na kuifanya mechi kuwa nzuri na mashabiki kufurahia soka safi. “Simba sasa inatakiwa kuangalia mbele zaidi ya hapo ilipofikia ikiwezekana kufanya vizuri katika uwakilishi wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Navas

The post Nahodha Sevilla aitabiria Simba makubwa Caf appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments