Windows

Mwadui bado waiota Ligi Kuu

. HAWAJAKATA tamaa. Kocha Mkuu wa Mwadui, Ally Bizimungu ameanza kujipanga kwa mechi ya mchujo kwa nia ya kuhakikisha wanasalia kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Mwadui waliomaliza nafasi ya 17 ikikusanya alama 44 imepangwa kuvaana na Geita katika play-0ff na Kocha Bizimungu amesisitiza lazima kieleweke kwani bado wanaitaka Ligi Kuu.


Bizimungu alisema licha ya ligi kuwa ngumu msimu huu, wanashukuru kutoshuka daraja moja kwa moja hivyo wanaenda kujiweka fiti kwa ajili ya mchezo huo.


“Bado tuna kazi ngumu kuhakikisha timu inaendelea kubaki kwenye ligi, tutajipanga kuwakabili Geita ili tusishuke daraja,” alisema Bizimungu.


Alisema hawajafikia malengo kwani hawajajihakikishia kucheza Ligi Kuu msimu ujao, hivyo tathimini itafanyika baada ya kumalizika kwa Ligi ya Mchujo.


Katika ratiba ya mechi hizo zinazochezwa Jumapili hii, Mwadui itaivaa Geita, na Kagera itacheza dhidi ya Pamba kabla ya kurudiana Jumamosi ijayo ya Juni 8.

Post a Comment

0 Comments