Windows

Mo Banka awapa presha Lipuli FC




NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO wa Yanga, Mohammed Issa ‘Mo Banka’, anaonekana kuwapa presha wapinzani wao Lipuli FC baada ya kocha wa kikosi hicho, Samwel Moja, kukiri yeye ndiye mchezaji atakayewasumbua.

Lipuli na Yanga wanatarajia kukutana Mei 6, mwaka huu katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), utakaopigwa kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Akizungumza na BINGWA jana, Moja ambaye aliushuhudia mchezo kati ya Yanga na Tanzania Prisons juzi, alisema Mo Banka amerejea katika kiwango chake hivyo kuifanya timu yake kuwa na mabadiliko makubwa.

Alisema uwezo wa kiungo huyo umesaidia kuimarisha eneo la katikati la kikosi cha Yanga hivyo kuwafanya waweze kumiliki mpira muda mrefu na kupeleka mashambulizi mbele, tofauti na alivyowaona kipindi cha nyuma.

“Nimeangalia mechi za Yanga za hivi karibuni nikabaini wameimarika sana eneo la katikati, hii imesababishwa na uwepo wa Mo Banka kulingana na uchezaji wake,” alisema Moja. Hata hivyo, alieleza kwamba kutokana na hali hiyo wanatakiwa kufanya kazi ya ziada wakati wa maandalizi ya mchezo huo, wakitambua wanakutana na Yanga ya tofauti kabisa na ile waliyoifunga katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Post a Comment

0 Comments