Windows

Mingange: Yanga hawatoki safari hii



KOCHA mkuu wa timu ya Azam Meja Mstaafu, Abdul Mingange, amewapa mapumziko ya siku mbili wachezaji wake kabla ya kurejea mzigoni kujiandaa kuikabili Yanga.

Azam itavaana na Yanga Mei 28, mwaka huu katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Mingange alitamba kwamba watachukua pointi tatu katika mchezo huo, huku akisisitiza mapumziko yatamalizika Jumamosi na kikosi kitarejea mzigoni kama kawaida.

“Nimewapa wachezaji mapumziko kwa sababu ligi inaelekea ukingoni na wamecheza muda mrefu bila kupumzika, ninatarajia watarudi na nguvu mpya.

“Tukianza mazoezi tutakuwa na siku tatu za maandalizi kabla ya kuivaa Yanga, ila hatuna wasiwasi kwa sababu ni mechi kama nyingine,” alisema Mingange.

Azam inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kukusanya pointi 72 ikicheza mechi 37, wakati Yanga ipo nafasi ya pili kutokana na alama 86 walizovuna.

Post a Comment

0 Comments