KOCHA Mwinyi Zahera wa Yanga ni kati ya watu tisa waliopelekwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa makosa ya nidhamu baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kuwasilisha malalamiko dhidi yao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na TFF, baadhi ya viongozi, makocha na wachezaji wamepekwa kwenye kamati hiyo sambamba na Zahera ambaye mara kadhaa amekunuliwa akiilalamikia TPBL hasa kuhusiana na viporo vya watani zao na waamuzi.
Mbali na Zahera, wengine waliopelekwa Kamati ya Nidhamu ni Athuman Bilal wa Stand United, Nassoro Mrisho (Geita Gold FC) na Ramadhani Nsanzurwimo (Mbeya City).
Viongozi ni Herry Chibakasa wa Friends Rangers, Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Walter Harrison (KMC) na Hussein Salehe wa Geita Gold wakati mchezaji aliyelalamikiwa ni Deus Tulusubya wa Pamba.
Kamati hiyo ya TFF inatarajiwa kukutana na kutoa maamuzi Jumapili ya wiki hii.
0 Comments