Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema mchakato wa usajili wa mshambuliaji Heritier Makambo uko katika mikono salama
Aidha Mwakalebelea amesema Yanga imepokea ofa nyingi zinazomuhusu mshambuliaji huyo
Amesisitiza bado hakuna mkataba uliosainiwa upande wa Yanga, hivyo amewahakikishia Wanayanga kuwa Makambo bado ni mchezaji wao halali
"Suala la Makambo liko mikono salama, uongozi tunalifahamu na tulitoa baraka zetu kwake pamoja na Mwalimu kwenda Guinea ambako alitakiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya," amesema
"Ilikuwa ni lazima aende na Mwalimu kwa sababu kule wanaongea kifaransa"
"Lakini ifahamike Makambo ana ofa nyingi, sio Horoya Fc pekee wanaotaka kumsajili, Jumatatu tutakutana na wengine"
"Tunazipitia ofa zote na kufanya tathmini kabla ya kuamua. Hakuna mkataba ambao umeshasainiwa kwa upende wetu. Na kwa kawaida mkataba lazima uwe wa pande mbili"
"Mpira ni biashara, kama kutakuwa na ofa nzuri tutafanya biashara lakini kama itakuwa tofauti basi tutaendelea kubaki na mchezaji wetu"
0 Comments