Windows

Manchester United yajiondoa kumuwania De Ligt



Manchester United imeachana na mpango wa kumuwania Mathhijs de Ligt, mlinzi wa kati wa Ajax ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo

Taarifa za awali zilibainisha kuwa baada ya FC Barcelona kusuasua kulipa dau la mlinzi huyo kinda ambalo ni Euro Mil 70, kikwazo kikiwa dau la wakala wake ambalo ni Euro Mil 14, Manchester United ilijitosa kumsajili ikiwa tayari kulipa fedha zote Euro Mil 84

Hata hivyo United imeachana na mpango huo ikitaja sababu kuwa mchezaji huyo mwenyewe anataka kujiunga na FC Barcelona

Uongozi wa United unaamini tayari mawazo ya beki huyo yako FC Barcelona

Post a Comment

0 Comments