


MANCHESTER United imeripotiwa kufanya mawasiliano na Antoine Griezmann wakipiga hesabu za kumsajili staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa anayesakwa pia na Barcelona katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.
Griezmann aliweka wazi hivi karibuni kwamba ataachana na Atletico Madrid mwishoni mwa msimu huu huku Barcelona wakipewa nafasi kubwa ya kumnyakua staa huyo aliyefunga mabao 133 katika mechi 257 alizochezea kwenye kikosi hicho kinachonolewa Diego Simeone katika michuano yote.
Lakini, baada ya sasa Barcelona kuonekana kama kusitasita hivi, Man United wameamua kuingia kazi kwenye mbio za kumsaka mshambuliaji wakiamini pesa za kumsajili staa huyo zipo.
Jambo zuri ni kwamba Real Madrid, Manchester City na PSG zote hazina mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo.
Thamani ya sasa ya Griezmann kwa kujibu wa kipengele kilichopo kwenye mkataba wake ni Pauni 173 milioni, lakini itashuka na kufikia Pauni 104 milioni kuanzia Julai Mosi.
Samuel Umtiti
ARSENAL wameripotiwa kuwa tayari kupeleka ofa yao huko Barcelona kwa ajili ya kumsajili beki wa kati Samuel Umtiti, lakini hilo litafanyika kama tu wataichapa Chelsea kwenye fainali ya Europa League. Kocha Unai Emery anataka kuimarisha safu yake ya mabeki kwa ajili ya msimu ujao hasa kama timu yake itakamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kitu ambacho kitatimia wakiifunga Chelsea wiki ijayo.



0 Comments