Yanga imefikia makubaliano na klabu ya Horoya Fc kumuuza mshambuliaji wake Heritier Makambo aliyesaini kunako klabu hiyo mkataba wa miaka mitatu
Habari njema ni kuwa Yanga itafanya biashara ya faida kwani itaingiza zaidi ya Mil 230, ikipata faida ya zaidi ya Mil 170
Makambo alitua Yanga akitokea klabu ya FC Lupopo ya DR Congo kwa dau la takribani Milioni 60
Yanga inaendelea na mchakato wa kukiboresha kikosi chake na bila shaka fedha hizo zitatumia katika usajili unaoendelea
cut
Makambo tayari ametambulishwa kunako klabu ya Horoya Fc, mabingwa wa Guinea
Mkurugenzi wa Ufundi wa Horoya Jaid Martin wiki ijayo atakuwa jijini Dar es Salaam kumalizana na Yanga ili kukamilisha taratibu za mwisho za usajili wa Makambo
Uongozi wa Yanga kupitia Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla amethibitisha kuwa na taarifa ya Makambo kwenda kufanyiwa vipimo vya afya
"Ni kweli Makambo aliondoka juzi na mwalimu Zahera kuelekea Guinea kwa ajili ya vipimo kwa klabu ya Horoya huko Guinea," amesema Dk Msolla
"Tunasubiri warudi tuitazame ofa yao kisha tufanye biashara. Taarifa za kutambulishwa rasmi sizielewi ila mwalimu akirudi tutaitazama ofa yao kulinganisha na klabu zingine nyingi zinazomtaka kisha tutafanya maamuzi"
Kwa habari zaidi Download App ya Mwana Jangwani kutoka Play Store. Bonyeza picha hapa chini
0 Comments