Windows

Dirisha la usajili Uingereza lafunguliwa mapema

Dirisha la Usajili nchini Uingereza lilifunguliwa rasmi jana May 16 na litafungwa August 08 2019

Tangu msimu uliopita Uingereza ilibadili taratibu za usajili kwa timu zinazoshiriki ligi kuu nchini humo ambapo dirisha la usajili litakuwa likifungwa kabla ya ligi kuanza
Nchi nyingine za Ulaya zinaendelea na utaratibu wa usajili kufunguliwa Juni/Julai na kufungwa Septemba 01
Inaelezwa utaratibu huu wa Uingereza utazinufaisha timu zao kwani zinaweza kuwahi kuwasajili wachezaji wazuri kabla ya timu nyingine kuanza michakato
cut
Msimu huu unatarajiwa kuwa na matumizi makubwa ya fedha kwa baadhi ya timu hasa Manchester United ambayo imejipambanua kutaka kukiimarusha kikosi chao ambacho kilimaliza nafasi ya sita
Manchester City imetangaza kutenga Pauni Milioni 200 kukiboresha kikosi chao kilichoibuka na ubingwa wa ligi kuu msimu uliomalizika
Arsenal, Tottenham, Liverpool nazo hazitakuwa nyuma kuboresha vikosi vyao
Chelsea haitaweza kusajili msimu huu kwa kuwa imefungiwa mpaka January 2020. Hata hivyo inaruhusiwa kuuza wachezaji ambapo inaelekea kumpoteza Eden Hazard anayewindwa na Real Madrid

Post a Comment

0 Comments