Windows

Kumbe Ngoma kauzibe!

UKISIKIA kauzibe ndio huku sasa, baada ya straika tegemeo wa Azam FC, Donald Ngoma kudai hakuna mchezaji yeyote kutoka Simba na Yanga anayeweza kukipiga katika timu hiyo kwa sasa, kama maisha yake ni kuhitaji usupastaa, huku akifichua anavyojisikia freshi. Ngoma aliyejiunga Azam mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga alikokuwa majeruhi wa muda mrefu, alisema maisha ya mastaa wengi wa Simba na Yanga yanatengenezwa na mashabiki na wanacheza kwa presha kwa kutaka kuwaaminisha kuwa wanastahili kucheza katika timu hizo na kudai ndio kilichowaharibu wachezaji wengi wazuri kwa kujisahau.


“Sina maana kwamba hakuna wachezaji wazuri katika klabu hizo, ila hawatamani kucheza Azam kwani haina mashabiki wengi na tayari wamelewa sifa wanafurahia mashabiki wanavyowapa kipaumbele zaidi na kusahau kuwa, kuna maisha mengine nje ya ushabiki.


“Kwa sasa huwezi ukamtoa mtu kama Ibrahim Ajibu aje Azam inayotegemea soka la uwanjani na sio mashabiki, ndio maana nasema hakuna anayeweza kuja kucheza huku kama hujitambui.” alisema Ngoma aliyefunga mabao 37 katika Ligi Kuu kwa misimu minne kuanzia mwaka 2015. Ngoma alisema amecheza Yanga na sasa yupo Azam na ameona tofauti kubwa baina ya klabu hizo, ila anafurahia kipaji chake kinachomfanya ajiachie kwa raha akifurahia maisha ya soka bila kujali kama kuna mashabiki wanamfuatilia au la.


Post a Comment

0 Comments