Windows

Kocha Azam amwaga visingizio

Picha

KOCHA msaidizi wa timu ya Azam FC, Idd Chehe amesema uchovu wa safari ni sababu iliyofanya kikosi hicho kuambulia pointi moja kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Stand United.

Mchezo huo wa 34 kwa Azam katika muendelezo wa ligi hiyo wajikuta wakivutwa shati na Stand United kwa kutoka sare ya bao 1-1 mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.

Matokeo hayo yamezidi kuwaweka njia panda wanalambalamba wanaoshika nafasi ya tatu kwa pointi 67 kwenye msimamo kwani sasa hata matumaini ya kumaliza wa pili yanayeyuka.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa pambano hilo juzi, Cheche alisema walijipanga kupata pointi tatu muhimu ili kuendelea hatma yao mbio za ubingwa lakini wameambulia moja na sababu moja wapo ni uchovu wa safari kwa wachezaji kutoka Dar es Salaam hadi Shinyanga.

“Mchezo ulikuwa mgumu kwetu pamoja na kutangulia kupata bao la mapema lakini wapinzani wetu walijitahidi kupambana na kipindi cha pili walisawazisha bao na kutufanya tupate pointi moja lakini kuchoka wachezaji ni sababu kubwa,” alisema.

Cheche alisema kwa kushirikiana na benchi la ufundi pamoja na kikosi hicho wanajipanga kuhakikisha michezo iliyobaki wanafanya vyema na kwamba pamoja na kupata matokeo hayo hawawezi kukata tamaa kwenye kuwania taji hilo msimu huu.

Kwa upande wa wapigadebe Stand wanaendelea kusalia nafasi ya 13 baada ya kufikisha pointi 40 kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 20 msimu huu baada ya

Post a Comment

0 Comments