Windows

Lipuli walituzidi- Zahera

Picha

KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema, kilichowafanya wapoteze mchezo wao mbele ya Lipuli FC ni wapinzani wao hao kuwazidi uwezo hivyo mbinu zao zote walizozitumia hazikufanya kazi.

Yanga walifungwa mabao 2-0 na Lipuli katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, FA, uliopigwa katika Uwanja wa Samora, Iringa juzi. Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo, kocha huyo raia wa DR Congo, alisema kuwa hakutarajia kama atakutana na upinzani mkali kama ule licha ya kuwajua Lipuli ni moja kati ya timu ngumu nchini.

Alisema kuwa mbinu alizoingia nazo aliamini kabisa zitawapa ushindi lakini kadiri muda ulivyozidi kusogea akaona wanapata wakati mgumu na kumlazimu kuzibadili. Alifafanua kuwa alifanya mabadiliko ya mfumo kwa kuwatoa Ibrahim Ajib, Haji Mwinyi na Mohammed Issa ‘Banka’ na kuwaingiza Amis Tambwe, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Juma Abdul lakini bado mambo yakawa magumu.

“Niliona Lipuli ni wagumu kufungika ndio maana nilimuingiza Tambwe, Juma na Ninja nikamtoa Ajib, Mwinyi na Banka ili kufanya tupandishe mashambulizi na kushambulia kwa kasi, tutumie mipira ya krosi kupata mabao lakini ikashindikana,” alisema Zahera. Kwa upande wa Kocha wa Lipuli, Seleman Matola alisema kuwa kilichowasaidia kupata ushindi katika mchezo huo ni kuzisoma mapema mbinu za Yanga.

Alisema kuwa walifanikiwa kuwadhibiti kila upande na kuutawala mchezo na kama wachezaji wake wangeongeza umakini wangeweza kupata mabao zaidi ya mawili lakini akawashukuru kwa kazi nzuri waliyoifanya kuipeleka timu fainali kwa mara ya kwanza. “Hii ni zawadi ya mashabiki wa Lipuli pamoja na watu wa Iringa kwa ujumla, tulitengeneza nafasi nyingi za kupata mabao lakini tukafanikiwa kufunga mawili, kwakuwa tumeenda fainali hayo tuliyoyapata yanatosha.

Post a Comment

0 Comments