Windows

Kabwili atamani soka la kulipwa

Picha

MLINDA MLANGO namba mbili wa Yanga Ramadhan Kabwili amesema anafikiria kwenda kucheza soka nje ya nchi kutimiza malengo aliyojiwekea kwenye maisha yake ya soka.

Kabwili alitoa kauli hiyo baada ya kuidakia timu yake kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Prisons uliochezwa uwanja wa Uhuru na Yanga kushinda mabao 2-1.

Alisema anaishukuru klabu yake na benchi la ufundi kwa kumuamini kusimama kwenye nafasi hiyo kwenye michezo mbalimbali ikiwemo ule wa watani wa jadi Simba amejifunza mengi na bado anahitaji kuendelea kujifunza hivyo ni wakati wa kwenda kucheza nje ya nchi kwenda kupata changamoto mpya.

“Ukiangalia kwenye kikosi cha Serengeti boys tuliowika kwenye michuano ya Afcon chini ya umri wa miaka 17 Gabon kwa asilimia kubwa wameenda kucheza soka nje ya nchi nimebakia mimi hivyo na mimi natakiwa kwenda kucheza nje, itakuwa mbaya zaidi kama nitaendela kubakia nchini,” alisema Kabwili.

Alisema maisha yake ni kucheza mpira na amejifunza mengi kwa kipindi kifupi alichocheza lakini bado anahitaji kujifunza mbinu mbalimbali ambazo zitamsaidia akiwa langoni kuendelea kujiamini .

Mkataba wa kipa huyo na Yanga unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na haijafahamika kama ataongezewa mwingine ama la.

Post a Comment

0 Comments