Beki wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya amesema moja ya sababu iliyowafanya washindwe kutamba msimu huu ni kutokufanya usajili dirisha dogo na kuamini vijana zaidi.
Kimenya alisema haikuwa kazi rahisi kuibakisha timu hiyo yote kutokana na usajili wao wa msimu huu kuwa tofauti na misimu miwili iliyopita.
Beki huyo amewaomba viongozi pamoja na kocha kutumia mapungufu waliyokuwanayo msimu huu kusajili wachezaji wazoefu na wenye uchu wa mafanikio ya haraka ili waweze kupata kikosi bora.
"Tulipoteana kabisa msimu huu dirisha dogo lilitumika kupandisha wachezaji vijana huku wengine wakiachwa kuondoka jambo ambalo naweza kusema liliivuruga timu kwa kiasi kikubwa na kufanya timu ishindwe kuwa na uelewano uwanjani."
"Kuna wachezaji walikuwa wanamaliza mikataba yao dirisha dogo la usajili waliruhusiwa kuondoka hakuna kitu kigumu kama kukutana na wachezaji wapya nusu ya timu uwanjani mnakuwa mnaenda tofauti kutokana na wengine kushindwa kumudu haraka mfumo wa mwalimu walioukuta," alisema Kimenya.

0 Comments