Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga kwenye uchaguzi uliomalizika wiki iliyopita, Yono Kevela leo amemkabidhi Makamu Mwenyekiti aliyechaguliwa Fredrick Mwakalebela fedha taslim Tsh Milioni 20 ikiwa ni mchango wake kwa klabu
Akikabidhi Mchango huo Makao Makuu ya Yanga, Kevela ametoa wito kwa Wanayanga kuichangia timu ili kuweza kuirejesha katika makali yake
"Wote tunapenda ushindi, sasa ni vyema wakati huu ambao timu yetu inapita katika kipindi kigumu tukashiriki kuisimamia," amesema
"Tuwajibike kuwawezesha viongozi wetu wapya ili waisimamishe timu na kuirejesha mahali pake"
"Naamini baadae timu ikishasimama na wawekeza kuja, tutaachana na utaratibu huu wa kutembeza bakuli"
Kevela amesema kiasi hicho cha fedha alichochangia iwe chachu kwa Wanayanga wengine kujitokeza na kuchangia kadiri ya uwezo wao

0 Comments