

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika klabu ya Yanga, Yono Kevela leo ametoa kiasi cha shilingi, milioni 20.
Kevela ametoa fedha hizo kwa uongozi mpya wa klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni.
Kevela ameamua kutoa fedha hizo ambazo zitakuwa sehemu ya mchango ndani ya klabu kwa ajili ya kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.
Fedha hizo zitasaidia katika masuala mbalimbali ya Yanga ikiwemo suala la usajili na mambo mengine.




0 Comments