SI umesikia kwamba Simba wamemtengea nahodha wa Yanga, Ibrahim Ajib, Sh milioni 85 katika usajili wa msimu uliopita? Sasa unaambiwa uongozi mpya wa Wanajangwani hao chini ya Dk. Mshindo Msolla, wamejibu mapigo.
Taarifa za uhakika kutoka Simba zinadai kwamba, wamemwekea mezani Ajib kitita hicho cha fedha ili kumrudisha nyumbani huku pia akiahidiwa mshahara mnono lakini Yanga nao wamekuja juu.
Kigogo mmoja wa Yanga ameliambia DIMBA Jumatano kuwa, uongozi mpya wa Wanajangwani hao umeamua kufanya mazungumzo na wachezaji wao wote wanaomaliza mikataba yao wakianza na Ajib.
“Taarifa hizi za Simba kumtaka Ajib tumezipata muda mrefu na hatukuwa na la kufanya kwa sababu hapakuwa na uongozi, lakini nikuhakikishie kwamba kila kitu kinakwenda vizuri kwa sasa.
“Tayari viongozi wapya wameingia msituni kuhakikisha wanawabakisha wachezaji wote wanaomaliza mikataba yao walioonyesha uwezo mkubwa na wanaanza na nahodha wetu Ibrahim Ajib,” alisema.
Alisema hawawezi kukubali kumwachia Ajib kienyeji kwani ametoa mchango mkubwa sana na yupo kwenye mpango wa kocha wao mkuu, Mwinyi Zahera, kwa ajili ya msimu unaokuja.
The post Jeuri ya Fedha yambakiza Ajibu Yanga appeared first on KWATA UNIT SPORTS & ENTERTAINMENT.
0 Comments