Windows

HONGERENI AZAM MEDIA, MMEIPAISHA TPL NA WACHEZAJI WA TANZANIA

mp

Mtangazaji wa Azam Tv Baraka Mpenja aka Sauti ya Radi akitangaza mpira wa miguu kati ya timu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam na timu ya Mbeya City kutoka jijini Mbeya katika mchezo uliofanyika jana kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Kulia ni Mtangazaji mwenzake Ahmed Ally wakiwa pamoja na mchambuzi wa mchezo huo.

……………………………………………………………………………….

Hapo awali wakati ligi mbalimbali zikionyeshwa kupitia kituo cha luninga  cha Super Sport ilikuwa ni vigumu sana timu za Tanzania na wachezaji kuonekana duniani kwa sababu ligi yetu ya TPL ilikuwa haionyeshwi katika kituo hicho cha Super Sport  ambacho ndicho maarufu zaidi Afrika kwa kuonyesha michezo mbalimbali barani Afrika na Ulaya pia.

Hii ililifanya soka letu kwa kiwango fulani kudumaa lakini pia wachezaji wetu walikuwa hawawezi kuonekana na kupata nafasi za kucheza mpira wa kulipwa katika mataifa mengine zaidi ya kwenda kucheza Uarabuni tu.

Baada ya Azam Media kuanzishwa na kuja na kituo chao luninga Azam Tv ndipo haswaa ligi yetu ilipoanza kujulikana katika nchi mbalimbali kutokana na kuoneshwa na kituo hicho, Pamoja na mambo mengine wachezaji wetu wakaanza kuonekana na kusambaa katika ligi mbalimbali Afrika na Ulaya,

Hili ni jambo la kujivunia sana,
Na niseme tu kwamba Azam Media imekuwa mkombozi wa soka la Tanzania kwa kiwango kikubwa sana na imesaidia wachezaji wetu kuonekana na kufuatiliwa na mawakala mbalimbali wa wachezaji jambo lililopelekea mafanikio kwa kiasi fulani kwa taifa letu kisoka,

Ndiyo maana hata ukiangalia majina ya wachezaji wa timu ya taifa (Taifa Stars) siku za hivi karibuni utakuta wanatajwa kutoka ligi mbalimbali barani Afrika na Ulaya kama vile Morroco, Misri, Afrika Kusini, Argeria, Botswana, Zambia, Ubelgiji, Hispania, Uingereza na kwingineko haya ni mafanikio makubwa ni imani yangu kupitia Azam Tv tutafanikiwa zaidi tuendako “HONGERENI AZAM MEDIA”


Post a Comment

0 Comments