![](https://4.bp.blogspot.com/-oWBF5rnYXzE/W7uedCj85EI/AAAAAAAAJdY/0jTfLk_9khU5DTaZ6o-KfH_A3hrpI_ZJQCLcBGAs/s320/aaaaaaaaaa.jpg)
![](https://1.bp.blogspot.com/-5UdUkBxLqPE/W7ujeNJL4XI/AAAAAAAAJds/dBugYDvLQq0WptS1YBXQGjJB_vJFBWL7wCLcBGAs/s320/yyyyyyyyyyyy.jpg)
Unajua mechi inayofuata wataicheza wapi? Wataifuata Singida United ambayo tangu irejee Ligi Kuu msimu uliopita haijawahi kuambulia japo pointi hata moja kwa mnyama, sasa kwa nini mashabiki wa Jangwani wasinune?
Kama wakishinda mchezo huo wa ugenini, kisha wakarudia kuikaribisha Ndanda na kupata tu sare, bila kujali matokeo ya Yanga, Simba itakuwa imetangaza ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo kwani itafikisha alama 89 na mabao ya kumwaga. Ushindi huo wa jana Alhamisiuliochagizwa na mabao ya nahodha John Bocco, Clatous Chama na Emmanuel Okwi, imeifanya Simba kufikisha jumla ya mabao 72 na kusalia bao moja tu kuifikia rekodi iliyowekwa na Yanga msimu wa 2015-2016 walipomaliza na mabao 73.
Katika mchezo wa jana, Kocha Patrick Aussems alianzisha majembe yote muhimu ambapo mbele aliwachezesha kwa pamoja, Okwi, Meddie Kagere na Bocco, huku kati wakisimama Jonas Mkude, Chama na Haruna Niyonzima.
Wakata Miwa waliosalia nafasi ya tano na alama zao 49 baada ya kuporomoshwa mwishoni mwa wiki na KMC, ndio walioanza pambano hilo kwa kasi na kufanya shambulizi hatari sekunde 56 wakati Riffat Khamis alipokaribia kuiandia timu yake bao baada ya kupigiana pasi za haraka haraka na Jaffar Kibaya lakini shuti lake lilitoka nje.
Shambulizi hilo liliwafanya Simba kucheza mpira wa umakini zaidi huku wakionyesha mipango dhabiti katika kushambulia ambapo Okwi, Bocco na Kagere walitengeneza nafasi kadhaa na kuisumbua ngome ya Mtibwa iliyokuwa chini ya kipa Shaaban Kado.
Dakika 22 John Bocco alipiga krosi mzunguko iliyomshinda kipa wa Mtibwa, Shaban Kado na mpira kutua miguuni mwa Okwi ambaye alipiga shuti kipa akiwa chini lakini umakini wa beki Dickson Daud aliokoa kwa kupiga shuti la mbali.
Mabeki wa Mtibwa, Cassian Ponela na Dickson Daud walikuwa wakicheza kwa maelewano na hata mmoja wapo alipokuwa anakosekana basi mkongwe Shabaan Nditi aliyekuwa anacheza kama kiungo mkabaji alikuwa anarudi nyuma na kuongeza nguvu.
Dakika ya dakika 32 Simba ilifanya shambulizi kali baada ya Meddie Kagere kupiga krosi kutoka upande wa kushoto na John Bocco aliumalizia kwa mguu wake wa kulia.
Bao hilo lililokuwa la 15 kwa Bocco msimu huu, liliwapa morali wachezaji wa Simba, baada ya kufanya shambulizi lingine dakika 34 kupitia kwa Nicolas Gyan aliyepiga krosi na Kagere kuunganisha kwa mguu hata hivyo mpira ulipita pembezoni mwa lango la wageni.
Dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili, Chama aliifungia Simba bao la pili baada ya Haruna Niyonzima kupiga pasi mpenyezo akiwa katikati ya uwanja na makosa ya Kado kutoka ovyo langoni kulimfanya Mzambia huyo kuusukua mpira kimiani.
Hilo lilikuwa bao la sita kwa Chama msimu huu na liliwaongezeka mzuka Vijana wa Msimbazi kwani dakika ya 57 Okwi alipachika bao la tatu na la 15 kwake msimu huu baada ya kupokea pasi kwa Jonas Mkude na shuti lake kumtoka mkononi kipa Kado. Simba walifanya mabadiliko dakika 60 kwa kumtoa John Bocco na kuingia Mzamiru Yassin, mabadiliko hayo yalimfanya Niyonzima kusogea upande wa kushoto na Mzamiru kucheza katikati, Mtibwa nao walijibu mapigo kwa kumtoa Chanongo na kuingia Ismail Aidan.
Mtibwa walifanya mabadiliko mengine dakika 70 kwa kumtoa Kibaya na kuingia Saleh Abdallah, mabadiliko hayo yalionyesha kushindwa kuisaidia timu hiyo kwani Saleh alienda kucheza kama kiungo mkabaji na kumfanya Riffat kusimama peke yake. Simba nao walifanya mabadiliko dakika 74 kwa kumtoa Kagere na kuingia Adam Salamba, kisha kumtoa Niyonzima na kuingia Hassan Dilunga dakika 82 kama njia ya kuibana zaidi Mtibwa ambao licha ya kufurukuta walijikuta wakimaliza dakika 90 kwa kipigo cha 3-0.
![](https://4.bp.blogspot.com/-oWBF5rnYXzE/W7uedCj85EI/AAAAAAAAJdY/0jTfLk_9khU5DTaZ6o-KfH_A3hrpI_ZJQCLcBGAs/s320/aaaaaaaaaa.jpg)
![](https://1.bp.blogspot.com/-5UdUkBxLqPE/W7ujeNJL4XI/AAAAAAAAJds/dBugYDvLQq0WptS1YBXQGjJB_vJFBWL7wCLcBGAs/s320/yyyyyyyyyyyy.jpg)
![](https://1.bp.blogspot.com/-5UdUkBxLqPE/W7ujeNJL4XI/AAAAAAAAJds/dBugYDvLQq0WptS1YBXQGjJB_vJFBWL7wCLcBGAs/s320/yyyyyyyyyyyy.jpg)
0 Comments