NA EMMANUEL MBATILO
Beki wa zamani wa Manchester United na timu ya Uingereza,Rio Ferdinand amemkosoa mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk kwa kuhusika katika bao la kwanza la Barcelona lililofungwa na Luis Suarez.
Ferdinand amesema Van Dijk alitakiwa kutembea na Suarez au kumshtua Matip kuhusiana na uelekeo wa mfungaji.
Ameyasema hayo baada ya usiku wa kuhamkia leo timu ya Liverpool kutembezewa kichapo kutoka kwa Barcelona katika raundi ya kwanza nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya (UEFA)
Liverpool alipigwa 3:0 ambapo Lionel Messi akifanikiwa kuingia kambani mara mbili wakati goli lingine likifungwa na mshambuliaji Luis Suarez.
0 Comments