Windows

Dah! Hatimaye Juuko aaga Simba

Mwanaspoti, Michezo blog, Hatimaye, Juuko, aaga, Simba, Mwanasport, Michezo
Beki wa Simba, Mganda Juuko Murshid ameaga rasmi mashabiki wa mabingwa hao wa Ligi Kuu bara baada ya kuichezea klabu hiyo kwa misimu mitano.


Juuko kwasasa yupo na kikosi chake cha timu ya Uganda 'The Cranes' kambi Abu Dhabi amemaliza mkataba na Wekundu hao wa Msimbazi.


Juuko ameichezea Simba kwa miaka mitano tangu alipojiunga nayo mwaka 2014 anaondoka kwenda kupambana na changamoto zingine kwani imedaiwa kuwa ana ofa na timu zingine huku ikitajwa moja ya nchi atakazokwenda ni Afrika Kusini.


Katika ukurasa wake wa Twitter, Juuko akiwa ameweka picha yake pamoja na Clatous Chama, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi aliandika; "Napenda kuwashukuru kwa kipindi chote kizuri tulichokuwa pamoja, ilikuwa ni safari nzuri kwani tulishirikiana pamoja ingawa wakati mwingine inatubidi kila mmoja kuwa mbali na mwingine,"


Mwaka jana, uongozi wa Simba ulimwongeza mkataba Juuko wa miezi sita ambao unamalizika sasa ingawa safari ya beki huyo inaweza kuwajumuisha wachezaji wengine waliomaliza mikataba yao na hawataongezwa akiwemo Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi.


Hivi karibuni, Okwi naye kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe wa kuaga ambao ulizua gumzo kwa mashabiki wa Simba, hata hivyo uongozi wa Simba kupitia Mwenyekiti wao Swedy Mkwabi alisema kwa wakati huo walikuwa hawajafanya mazungumzo yoyote ya kumwongeza mkataba mpya.Nyota wengine wa kigeni wanaotajwa kutemwa ni Nicolaus Gyan, Zana Coulibaly, Asante Kwasi, Pachal Wawa pamoja na Haruna Niyonzima ambaye majadiliano yanaendelea kwani inadaiwa kocha Patrick Aussems amempendekeza msimu ujao lakini viongozi hawajaafiki.





Post a Comment

0 Comments