


AWALI, ilionekana kuwa Liverpool ndiyo inayoweza kumchukua kirahisi staa wa Lyon, Nabil Fekir, kwa kuwa walikaribia kumchukua wakati wa usajili wa Januari, mwaka huu.
Lakini sasa, Manchester City nao wamezama, ikisemekana kuwa wamepeleka ofa yao kwa mabosi wa Lyon.
Fekir raia wa Ufaransa, alikuwa na msaada mkubwa kwa Lyon msimu uliokwisha hivi karibuni, akifunga mabao 12 na kutoa asisti nane katika mechi zake 39.



0 Comments