

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwanoa mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo
Uamuzi wa kumuongezea mkataba umefikiwa na Bodi ya Wakurugenzi baada ya Kocha Aussems kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni
Kwenye mkataba huo Aussems alitakiwa kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu na inafika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika



0 Comments