

Hakuna kitu ambacho kitawaumiza mashabiki wa Simba kama mshambuliaji wao hatari Emmanuel Okwi ataondoka msimu huu
Okwi amekuwa akihusishwa na timu kadhaa kutoka Afrika Kusini. Mkataba wake uko mwishoni na inaelezwa bado hajasaini mkataba mpya
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram Okwi ameweka ujumbe 'tata' ambao unaweza kuwa na ishara ya kuwaaga mashabiki wa Simba
Katika ukurasa huo Okwi ameandika :
"Kwa heri ndio neno la huzuni zaidi.."
Hata hivyo uongozi wa Simba bado haujatoa taarifa yoyote kuhusu mshambuliaji huyo kipenzi cha Wanamsimbazi
Inaelezwa kumekuwa na mazungumzo yanayoendelea ili kuhuisha mkataba wa mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Uganda



0 Comments