YANGA, leo Ijumaa itakuwa mkoani Mara kwa ajili ya kusaka pointi tatu ili kukimbizana na Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara lakini kikosi hicho cha Kocha Mwinyi Zahera kitacheza bila ya nahodha wake, Ibrahim Ajibu ambaye ameachwa jijini Dar.
Ajibu hatakuwa kwenye kikosi hicho wakati kitakapopambana na wenyeji wao, Biashara United kutokana na kuumwa malaria ambayo imemfanya abaki Dar kwa ajili ya matibabu. Yanga wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 80, leo watakuwa wenyeji wa Biashara kwenye Uwanja wa Karume, Mara.
Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kwamba Ajibu alipata ugonjwa wakati wakijiandaa kwenda mkoani humo ambapo baada ya kupata huduma ya kwanza kutoka kwa daktari wa timu hiyo, Edward Bavu imeonekana ana malaria, hivyo kuamua kumuacha.
“Kikosi chote cha wachezaji ambao walitoka kwenye mechi yetu ya Kombe la Shirikisho mkoani Iringa wapo vizuri hadi tunafika hapa, kasoro Ibrahim Ajibu ambaye yeye hatakuwa sehemu ya mechi hii ya kesho (leo).
“Wakati tunaondoka kuja huku Ajibu akapata ugonjwa wa ghafla akawa anatapika, baada ya dokta kumpa huduma ya kwanza ikaonekana ana malaria, hivyo amebaki Dar lakini wachezaji wengine wote wapo vizuri,” alisema Hafidh.
SPOTI HAUSI: AUSSEMS Kumkosa NIYONZIMA Simba SC
The post Ajibu awekwa kando Yanga, aachwa Dar appeared first on Global Publishers.
0 Comments