NAHODHA wa Yanga, Ibrahim Ajibu, amesema kuwa ngoma ya ubingwa bado mbichi, hivyo kasi yake lazima iendelee mpaka wapate kile wanachostahili kwenye Ligi Kuu Bara.
Ajibu ndiye kinara wa kupiga pasi za mwisho akiwa nazo 16 na ametupia mabao sita hali ambayo inamfanya azidi kuwa injini ndani ya kikosi cha Yanga.
Akizungumza na Championi Jumatano juzi baada ya kutoa pasi yake ya 16 kwenye mchezo dhidi ya Azam ambao timu yake ilishinda bao 1-0, Ajibu alisema kuwa kikubwa kinachomfanya kuwa bora siku zote ni ushirikiano ambao anaupata kutoka kwa wachezaji.
“Ushirikiano uliopo kati yetu wachezaji pamoja na benchi la ufundi unatufanya tunakuwa bora siku zote na tuna nia ya kupambana ili kufi kia malengo yetu ambayo tumejiwekea kwa pamoja.
“Kila baada ya mechi kumalizika tunaanza maandalizi ya mchezo mwingine, kazi bado inaendelea kwa sasa kwani ligi haijaisha na ushindani ni mkubwa, maelekezo ambayo tunapewa na kocha wetu, Mwinyi Zahera yanatufanya tunakuwa bora, hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti hadi mwisho wa msimu, nitaendelea kupambana,” alisema Ajibu.
Michezo waliyobakiwa nayo Yanga kwa sasa ni dhidi ya Tanzania Prisons, Biashara United, Ruvu Shooting, Azam FC na Mbeya City.
0 Comments