Windows

UCHAGUZI YANGA MPAKA KIELEWEKE, WANACHAMA WATAKIWA KUJITOKEZA KUCHUKUA FOMU, RATIBA IPO NAMNA HII

MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahela amewataka wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili kugombea uongozi ndani ya Yanga.

Mchungahelea amesema kuwa uchaguzi ni muhimu kufanyika na kwa namna yoyote ile safari hii hakuna kitakachoukwamisha uchaguzi huo.

"Uchaguzi wa Yanga ni lazima ufanyike mwaka huu Mei, 5 hivyo wanachama wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu," amesema Mchungahela.

Hii hapa ratiba kamili ya nchakato wa uchaguzi Yanga. 

Aprili 2-7 kuchukua fomu

Aprili 9 Kikao cha mchujo kwa wagombea

Aprili 10 kubandikwa kwa majina yaliyopitishwa

Aprili 11-14 Pingamizi kwa wagombea

Aprili 16-18 Kupitia pingamizi na usaili

Aprili 18-23 Sekretariati kusikiliza maamuzi ya kamati ya maadili

Aprili 24-26 Kukata rufaa

Aprili 27-29 kusikiliza rufaa

Aprili 30- Mei 4 Kampeni 


Mei 5 uchaguzi mkuu.

Post a Comment

0 Comments