KOCHA wa Ruvu Shooting, Abdulmutik Haji amesema kuwa watapambana katika mchezo wao wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar kubeba pointi tatu zitakazowafanya wawe kwenye nafasi bora kwenye ligi.
Haji amesema watatumia vema uwanja wa nyumbani wa Mabatini kuwapapasa wapinzani wao Mtibwa Sugar.
"Mchezo utakuwa mgumu hasa kwa namna ligi inavyokwenda kwa sasa kila timu inapigana kupata pointi tatu muhimu, hilo limetufanya tujipange kikamilifu kushinda mchezo wetu.
"Wapinzani wetu tunawajua wapo vizuri ila hakuna namna nyingine ambayo tunatakiwa kufanya zaidi ya kupata pointi tatu, tupo kwenye nafasi ambayo hairidhishi ila kwa namna tulivyopishana kwa pointi chache nikishinda tu naibukia kwenye kumi bora," amesema Haji.
Ruvu Shooting ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 31 imejikusanyia jumla ya pointi 35 huku wapinzani wao Mtibwa Sugar wakiwa nafasi ya 6 baada ya kucheza michezo 29 na wana pointi 41.
0 Comments