Windows

JKT TANZANIA YAPANIA KUISAMBARATISHA SIMBA MAZIMA LEO


KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abdallah Mohamed 'Bares' amesema kuwa kazi yake ya kwanza leo atabeba pointi tatu muhimu mbele ya Simba ili kurejesha heshima ya JKT Tanzania.

Bares kabla ya kuinoa JKT Tanzania alikuwa kocha wa Prisons alipigwa chini kwa kile walichoeleza kuwa na matokeo mabovu, amejiunga na JKT Tanzania hivi karibuni akichukua nafasi ya Bakari Shime aliyesimamishwa kwa muda.

Bares amesema amekaa na timu kwa muda mfupi ila ana imani kwa mbinu alizowapa wachezaji wake pamoja na kuwasoma wapinzani wake mbinu zao ana uhakika ataibuka na pointi tatu muhimu.

"Muda mchache nimekaa na timu ila nimegundua wachezaji wana uwezo mkubwa na morali yao ipo juu, wapinzani wangu Simba nawatambua nimewafuatilia na kuzinasa mbinu zao hivyo hawanitishi ninaanza nao.

"Nimewaambia vijana, wachezaji wa kulindwa ni wote na sio kumtazama Bocco (John), Kagere (Meddie)  wala Chama (Clatous) bali ni timu nzima kwani wapinzani wetu wana mbinu nyingi ila hilo halinitishi," amesema Bares.

JKT Tanzania kwa sasa ipo nafasi 13 baada ya kucheza michezo 31 ikiwa na pointi 36, mchezo wao wa kwanza walipoteza nyumbani Mkwakwani kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba.


Post a Comment

0 Comments