Windows

OKWI, CHAMA WAUNGANA NA WENZAO MOROGORO TAYARI KWA KAZI







Mshambuliaji Emmanuel Okwi pamoja na king Cleotus Chama wameungana na wenzao kambini mjini Morogoro.



Chama na Okwi wametua mjini Morogoro, Simba ikiwa katika maandalizi ya kuivaa JKT Tanzania keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


Wawili hao hawakuwa kambini wakati Simba ikiwa mjini humo katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Mbao FC.

Mechi hiyo, Simba ilionyesha kandanda safi na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.


Post a Comment

0 Comments