

Mwanariadha nguli wa Uingereza Mo Farah amesema kushinda mbio za mwaka huu za London Marathon kutakuwa ni mafanikio sawa na mataji ya Olimpiki na sita ya dunia aliyoshinda.
Farah mwenye umri wa miaka 36 mzaliwa wa Somalia – ambaye aliangazia mbio za marathon baada ya kunyakua fedha katika fainali ya mita 5,000 jijini London 2017 – atakuwa na sababu nzuri ya kuyaweka katika kiwango cha juu kabisa mashindano hayo mwaka huu kwa sababu anastahili kumpiku anayeshikilia rekodi ya ulimwengu na bingwa mtetezi wa London marathon Eliud Kipchoge.
Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 34 – aliyepewa ushindani mkali na Farah mwaka jana kabla ya Muingereza huyo kumaliza katika nafasi ya tatu – anaiwinda rekodi ya ushindi wa nne kwa wanaume katika mbio hizo Jumapili ijayo. “Lengo langu ni siku moja kushinda London Marathon,” alisema Farah.
“Hilo ndio lengo langu lakini hauwezi kuichukulia kwa urahisi tu kwa sababu Eliud ni mwanariadha mzuri sana na anayeshikilia rekodi ya dunia. Kama ntampiku, yatakuwa mafanikio muhimu.” Alisema Farah. Mwanariadha huyo wa Uingereza anasema ushindani wake na Kipchoge ni muhimu katika mchezo huo wa riadha.



0 Comments