Windows

KCCA yarudisha nyumbani taji la ligi Kuu ya Kandanda Uganda

Klabu ya Kampala Capital City Authority FC (KCCA) ndio mabingwa wa ligi kuu ya kandanda nchini Uganda baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na Ndejje University, mtanange uliochezwa uwanja wa Arena of Visions. Sare hiyo imeifanya timu hiyo kufikisha alama 60, 7 zaidi ya timu iliyopo nafasi ya pili Vipers.

Wakiwa katika jezi zisizozoeleka na mashabiki wa timu hiyo, za rangi ya kijani, KCCA wametangazwa kuwa mabibgwa wapya msimu wa 2018/2019.
Unakuwa ubingwa wa 13 kwa KCCA tangu ilipoanzishwa mwaka 1949 na kuingia kwenye klabu zenye mafanikio zaidi nchini Uganda.

Ibrahim Sadam Juma aliyeingia kama mchezaji wa akiba kwa upande wa KCCA alifanikiwa kufunga goli dakika ya 60 na kufuta goli la mapema la Anwar Ntege huku klabu ya Vipers wakishinda dhidi ya Lugogo 2-1.

Matokeo ya sare ambayo KCCA iliyapata dhidi ya Ndejje University yanaipelekea timu hiyo kushuka daraja mwa ligi hiyo.

KCCA walianza mara ya kwanza kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uganda mwaka 1976.

Baadae neema ya taji hilo ilifuatia ikiwa imetwaa kwa mara 12 kama ifuatavyo 1977, 1981, 1983, 1985, 1991, 1997, 2008, 2013, 2014, 2016, 2017 na sasa mwaka 2019 imefanikiwa kunyakua tena taji hilo.

Zimebakia mechi mbili kumalizika msimu huu. Changamoto kubwa kwa KCCA kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye mashindano ya CAF kwani mpaka sasa imekuwa kama mshiriki na sio mshindani kufika hatua ya robo au nusu fainali sio kombe la shirikisho wala Ligi ya Mabingwa.


Post a Comment

0 Comments