Windows

MBEYA CITY WAPANIA KULIPA KISASI LEO MBELE YA KMC, SOKOINE MBEYA


KOCHA wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Sokoine saa 10:00 jioni.

Mbeya City wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza uliochezwa Uhuru kwa kufungwa bao 1-0.

"Tupo tayari kwa ajili ya kupambana na tunahitaji pointi tatu leo, mchezo wa kwanza tulipoteza ila leo tupo nyumbani tutatumia vema uwanja wa nyumbani, mashabiki watupe sapoti," amesema Nsanzurwimo.

Mbeya City wamecheza michezo 29 na wamekusanya pointi 37 wapo nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi.


Post a Comment

0 Comments