Windows

LIONEL MESSI APATA MAJERUHI, KUIKOSA MANCHESTER UNITED


MSHAMBULIAJI wa timu ya Barcelona, Lionel Messi ataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali dhidi ya wapinzani wake Manchester United kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Messi ambaye alianza kupata majeruhi kwenye mchezo wa kimataifa wakati akiitumikia timu yake ya Argentina dhidi ya Venezuela na kupewa matibabu kisha akaibukia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya wapinzani wake Espanyola.

Kwenye mchezo huo Messi alionyesha maajabu kwa kufunga mabao muhimu mawili moja alifunga kwa faulo ya mtindo wa paneka.

Messi aliumia jana akiwa na timu yake ya Barcelona alipokuwa kwenye mazoezi ya kujiaandaa na mchezo dhidi ya Villarreal ambao utachezwa leo.

Imeelezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili ambapo atakosa michezo mitatu ambayo ni miwili ya ligi dhidi ya Atletico Madrid na Huesca huku mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United.

Post a Comment

0 Comments