KOCHA wa Azam FC, Idd Cheche leo atakuwa kazini akimenyana na Kagera Sugar, Uwanja wa Nyamagana mchezo wa ligi kuu.
Mpaka sasa tayari Azam imecheza mechi 5,ikiwa chini ya Cheche na kufanikiwa kushinda zote ikijikusanyia jumla ya mabao 17 na kuruhusu kutingishwa nyavu zao mara mbili tu.
Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo ni mkubwa ila wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.
"Mwendo wa kutafuta pointi tatu muhimu unaendelea tunawaheshimu wapinzani wetu na tunawatambua kutokana na kucheza nao ila matokeo yaliyopita ni historia sasa tunafungua ukurasa mwingine," amesema Alando.
Azam FC wapo nafasi ya pili kwenye ligi wakiwa na pointi 59 bada ya kucheza michezo 28 huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 67.

0 Comments