Windows

MANARA: WACHEZAJI 100 WAMEOMBA KUICHEZEA SIMBA





Simba wamepata maombi ya wachezaji wapatao 100 wanaopendelea kuichezea nje.


Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wachezaji wanaotaka kuichezea Simba wanatokea ndani na nje ya Tanzania.


“Tena wengine wameandika barua wakionyesha kuwa na nia ya kuja kuichezea Simba. Lakini kuna utaratibu a alum wa benchi la ufundi ndio wanajua wanamhitaji nani,” alisema.


Kwa sasa, Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ndio timu yenye mvuto zaidi kutokana na kufanya vizuri zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.



Post a Comment

0 Comments